Skip to main content

Diamond Platnumz Awakimbiza Wizkid , Burna Boy Tuzo za BET


Nyota wa muziki kutokea nchini Tanzania, Naseeb Abdul Juma maarufu kwa jina Diamond Platnumz ameonekana kupata muitikio mkubwa kwenye post za wasanii wa Afrika aliokutana nao kwenye kipengele cha "Best International Act" kwenye tuzo za BET 2021.



Diamond amepata muitikio wa idadi kubwa ya maoni na 'likes' kwenye post za Instagram za wiki iliyopita za ukurasa wa 'Bet Africa' tofauti na wasanii wengine wa Afrika aliokutanishwa nao kwenye kipengele hicho cha tuzo.





Diamond akiwa ni msanii pakee kutokea Afrika Mashariki kuteuliwa kuwania tuzo hizo, wasanii aliokutanishwa nao kutoka Afrika ni pamoja Burnaboy, Wizkid.



Kwenye kupengele hicho cha 'Best International Act', Diamond Platnumz mbali na Diamond  kukutana na wasanii hao kutokea nchini Nigeria pia amekutanishwa na Aya Nakamura (France), Emicida (Brazil), Headie One (Uk), Young T & Bugsey (Uk) na Youssoupha (France).




Hii ndiyo Orodha ya Wasanii Wanao Wania Tuzo hii Na Diamond Platnumz

Hata hivyo, hafla ya utoaji wa tuzo hizo maarufu na zenye heshima Duniani itafanyika Juni 27 2021.





Comments