Skip to main content

Sergio Ramos Afunguka Mwanzo Mwisho Sababu za Kuondoka Real Madrid

Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa nahodha wake Sergio Ramos ataondoka klabuni hapo katika dirisha la usajili la majira ya joto (Summer) baada ya kuhudumu klabuni hapo kwa miaka 16. Awali Madrid walituma ofa ya mwaka mmoja huku nyota huyo akitaka angalau mkataba wa miaka miwili.



Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameweka wazi kuwa, wakati makubaliano ya mkataba mpya na Ramos hayakufikiwa na kusisitiza kuwa Sergio Ramos ataendelea kukaribishwa tena klabuni hapo kwa siku za usoni.


Katika sherehe za kumuaga Sergio Ramos zilizofanyika Madrid siku ya jana. Ramos amefunguka ukweli wote ikiwemo taarifa ya kuomba apewe mkataba mpya tangu 2018 baada ya fainali za michuano ya UEFA mwaka huo , Lakini Perez alikuwa akitoa ahadi hewa. Unaambiwa katika zama za Perez hakuna Legend aliyestaafu akiwa na jezi ya Real Madrid.


MKUTANO WA SERGIO RAMOS NA WAANDISHI WA HABARI

Real Madrid walitaka kunipa mkataba mpya nami nilikubaliana nao, ukiwa na kipengele cha kupunguza mshahara kwa 10% , Sikuwa na pingamizi kwenye ombi hilo kwakuwa pesa haikuwa kipaumbele changu, nami nikawaomba mkataba wa miaka miwili.


Kwa bahati mbaya sana klabu iligoma kusikiliza wao walitaka wanipe mwaka mmoja pekee, sikujisikia vizuri kwenye hilo , Nilitazama namna nimepambania klabu, haikuwa kama upendeleo bali nilistahili mkataba wa miaka miwili.



Lakini kwa mapenzi yangu kwa hii klabu nikawaomba nikaifakari ofa ya mwaka mmoja walionipa kisha nitarejea , Baada ya tafakuri nilirejea baada ya muda kupita, nikawaambia nipo tayari kukatwa mshahara na kusaini huo mwaka mmoja.


Majibu niliyopewa ni kuwa, muda wa kusaini huo mkataba ulishapita hivyo nitafute timu ya kucheza , Binafsi wakati tunaachana kwa mara ya kwanza kwenda kutafakari hawakuniambia kama kuna muda maalum, bali nikiwa tayari nikasaini , Tayari yameshatokea, siondoki Madrid kisa pesa bali sikupewa mkataba mpya. Asante Real Madrid kwa kila kitu, nitaibeba hii klabu moyoni mwangu na naamini siku moja nitarejea tena hapa.



Sergio Ramos , Amesema maneno hayo wakati akiwa anaaga mbele ya Rais Perez, Jijini Madrid. Inasemekana anaenda klabu ya nje ya Hispania na bado haijatajwa wazi mpaka hivi sasa.


Comments