Mkongwe wa WWE John Cena usiku wa Jana alirejea tena Kwenye kampuni hiyo Baada ya kukaa Nje ya mchezo Huo kwa Muda wa mwaka mmoja na nusu , Kurudi kwake kumeifanya WWE kurejea kwa Kishindo huku John akikiri kwamba Amerejea katika Mchezo huo kuuchukua Utawala wa Mashindano hayo Makubwa nchini Marekani.
Awali Roman Reigns aligoma Kupigana na John Cena kwenye kipindi cha Smack Down wiki iliyopita na kukubali kupambana na Mpinzani mwingine Finn Balor kisha John Cena akatokea na Kuchukua nafasi ya Finn hivyo Mpambano rasmi utakuwa Agosti 21 mwaka 2021.

Comments
Post a Comment