Skip to main content

Kanye West Atunukiwa Heshima Katika Jiji la Atlanta ' Julai 22 Yatajwa Kuwa Siku Ya KANYE WEST

Masaa machache Kabla ya Kanye West kuingia Jukwaani Katika Uzinduzi wa albamu ya DONDA, Rapa huyo alijikuta Akipokea heshima kutoka kwa uongozi wa Jiji la Atlanta kwa kumtunuku siku ya tarehe 22, Julai kila Mwaka katika jiji hilo kuwa siku ya KANYE WEST.




Katika Uzinduzi wa Awali wa albamu hiyo Usiku wa Jana ' Wakaazi wa Jiji la Atlanta walifanikiwa Kuujaza uwanja wa Mercedes Benz kwa Lengo la kuisikiliza Albamu ya DONDA huku Kwa mara ya Kwanza baada ya Kitambo rapa Jay Z atasikika tena Katika moja ya Nyimbo zinazopatikana Katika albamu hiyo ' Pia mwanamama Kim Kardashian akiwa Ameongozana na Watoto wake North , Saint , Chicago , and Psalm walikuwepo Katika kuisikiliza Albamu hiyo.




Kanye West alizaliwa huko Atlanta na aliishi Katika jiji hilo hadi Alipokuwa na miaka Mitatu kufuatia wazazi wake Kuachana.  Baba yake anaitwa Ray West, alikuwa mwandishi wa picha na Jarida la Atlanta na Mama yake, marehemu anaitwa Donda West, alikuwa Profesa wa Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Clark Atlanta na Chuo cha Morris Brown.




Comments