| Jay Willz akiwa Na Diamond Platnumz |
Mwaka 2022 umeanza kwa kasi sana kwa mwanamuziki Diamond Platnumz kutokana na kazi zake za Muziki , Baada ya kumaliza kolabo na The Ben kutoka nchini Rwanda Diamond sasa Amevuka mipaka mpaka nchini Nigeria.
Nyota huyo ambaye ni mkurugenzi wa lebo ya muziki WCB Wasafi kwa sasa Yupo nchini Nigeria akiwa anakamilisha video na msanii wa muziki kutokea nchini humo anayeitwa Jay Willz ambaye anatamba na wimbo wake unaoitwa Medicine aliouachia tangu Agost 25, 2021.
Kupitia ukurasa wake wa katika mtandao wa Instagram Jay Willz amechapisha picha akiwa na Diamond katika moja ya Eneo ambalo wanatayarisha video Hiyo na kuambatanisha maneno yaliyosomeka “Diamond Platnumz feat Rolly Boy Big 2022”
Diamond Platnumz ametua Nchini humo kimya kimya kukamilisha kideo hicho na Huku akiwa na shughuli zingine za kimuziki katika taifa hilo.
Comments
Post a Comment