Mkurugenzi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza kuingia kwenye fani ya uigizaji wa filamu muda wowote kuanzia sasa.
Kondeboy ameweka wazi hilo kupitia Insta Story yake ambapo amebainisha kuwa filamu hiyo kwa mara ya kwanza itaoneshwa kupitia mtandao wa Ceek , Kampuni ambayo inajihusisha na masuala ya burudani kama kurusha matukio ya mubashara mtandaoni, kuandaa matamasha, kutengeneza headphones n.k
Harmonize ameandika “Nimechoka kusubiri filamu yangu ya kwanza. Itakuwa kali sana, tukutane Ceek hivi karibuni jisajili sasa” - Harmonize
Comments
Post a Comment