SIMBA , Diamond Platnumz amejiwekea rekodi nyingine baada kutumbuiza kwenye tamasha maalum lililoandaliwa na waandaaji wa tuzo za Grammy na kumfanya kuwa msanii wa kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kutumbuiza kwenye show hiyo inayokwenda kwa jina la Global Spin
Show hii ambayo huwa inaruka mubashara kwa njia ya mtandao kupitia YouTube , Twitter , Facebook za Recording Academy ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2021 ikiwa na lengo la kuibua na kuutangaza zaidi muziki wa Afro Beat K-Pop na Latin Music
Diamond pia ameutambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa Jina la Gidi katika show hiyo , Huku akichanganya vionjo vya wimbo wa Wizkid unaoitwa Show You The Money

Comments
Post a Comment