Skip to main content

Harmonize Awaondoa Jux , Darassa Afro East Carnival

Mkurugenzi wa lebo ya Konde Music World Wide Harmonize amewaondoa wasanii Jux na Darassa katika orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Afro East Carnival baada ya wakali hao kudai kuwa hawana makubaliano yoyote Juu ya kuwepo kwao kwenye tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Harmonize litakalo fanyika tarehe 05 March 2022 maeneo ya Tabata Shule.


Kupitia Empire ya Efm Jux amesema kuwa yeye binafsi (Jux) alimtafuta Konde Boy na kumuelezea hatua alizozipitia kwenye makubaliano hayo kuwa sio Sahihi lakini hawakuchukulia serious inshu hiyo.

Jux ameeleza kuwa , Ni kweli Harmonize aliwahi kumtafuta na kumuelezea kuhusu Afro East Carnival , na baada ya hapo hawakuzungumza lolote kuhusu malipo na ratiba yake , Ila walichokubaliana ni kwamba vitu vikiwa tayari waambiane kwa ajili ya mikataba zaidi , Ila Jux anasema kuwa siku ya leo aliamka na kukuta tangazo limewekwa tayari kuwa atakuwepo kwenye show hiyo.


AfricanBoy ameongeza kuwa baada ya kuliona Tangazo , Aliutafuta Uongozi wa Konde Music lakini hakupewa majibu yanayoridhisha , Kisha alimtafuta Harmonize mwenyewe na kumueleza na hata baada ya hapo Tangazo hakulitoa na aliliacha liendelee kuwepo kwenye Page yake.

African Boy amesema kuwa kitendo hicho sio sawa kwenye muziki na biashara yake , hivyo haelewi ushikaji unapitiliza au kumchukulia poa au kama dharau kwa upande wake.

Comments