Skip to main content

Hamisa Mobetto Alamba Dili la Mamilioni , Kukaa Meza Moja Na Blac Chyna

Mwanamitindo na mjasiriamali kutokea nchini Tanzania, Mwanadada Hamisa Mobetto amesaini dili nono la ubalozi wa vipodozi vya Whitenicious kwa upande wa Bara la Afrika akimsaidia mwanadada Blac Chyna kutoka nchini Marekani ambaye ni balozi wa bidhaa hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa ametambulisha Ubalozi huo na kuandika “Hatimaye siri ya urembo wangu ni hii. Ningependa kutangaza rasmi kwamba nimekuwa balozi wa Whitenicious Afrika. Kwa kushirikiana na Whitenicious nitatangaza urembo kwa kutumia bidhaa za asili kwaajili ya wanaume na wanawake. Kwa miaka mingi Afrika imekuwa ikipokea bidhaa za urembo zenye kemikali. Bidhaa hii inamiaka 30 sokoni ikihakikisha ngozi za wanawake na wanaume zikiwa salama” - Hamisa Mobetto

Mrembo huyu ukiachilia mbali dili hili la vipodozi vya kimataifa, Milango ya kibiashara inazidi kufunguka kwani pia ni balozi wa kinywaji cha Belaire.

Comments