Waandaji wa Tuzo za #Oscar wamelaani Kitendo kilichofanywa na Muigizaji Will Smith usiku wa Jana katika Ugawaji wa Tuzo hizo.
Academy wamesema Kuwa wanafuatilia kwa Ukaribu tukio hilo na Watatoa maamuzi Makali kwa Mujibu wa Sheria zinavyosema.
Smith ameingia Kwenye vichwa vya Habari baada ya Kumpiga kibao shavuni Mchekeshaji Chris Rock kwenye Jukwaa la Tuzo hizo Kutokana na Utani wa Rock kwa Jada Pinkett Smith's ambaye ni Mke wake aliposema Kuwa nywele za Mwanamama huyo ni Mbaya kwa sababu Anaelekea kuwa na Kipara.
Pinkett Smith alishawahi Kusema kuwa Ana tatizo Lijulikano kitaalamu Kama Alopecia (Hali ya Kupoteza nywele Kichwani.



Comments
Post a Comment