Skip to main content

Mtoto wa Kiume wa Cristiano Ronaldo Afariki Usiku wa Jana

Mshambuliaji wa Manchester United raia wa Ureno , Cristiano Ronaldo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ametangaza kuwa mmoja wa mapacha wake wachanga amefariki dunia siku ya jana.


Forexmart
Chapisho hilo la Ronaldo lilisomeka “Ni kwa masikitiko yetu makubwa tunalazimika kutangaza kwamba mtoto wetu wa kiume ameaga dunia. Ni maumivu makubwa zaidi ambayo wazazi wowote wanaweza kuhisi. Kuzaliwa tu kwa mtoto wetu wa kike kunatupa nguvu ya kuishi wakati huu kwa matumaini na furaha..


Tungependa kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa huduma na usaidizi wao wote wa kitaalam. Sote tumehuzunishwa na tunaomba faragha katika wakati huu mgumu sana..


Mtoto wetu wa kiume, wewe ni malaika wetu. Tutakupenda daima.” –Imeeleza taarifa hiyo.

Comments