Skip to main content

Burna boy Aweka Rikodi mpya Africa , Aingiza Dola $7,276,150 kwa Usiku mmoja

Nyota wa muziki kutokea nchini Nigeria African Giant , Burna Boy ameingiza mabilioni ya fedha kutoka kwenye tamasha alilolifanya siku chache zilizopita Madison Square Garden , New York.

Damini Ogulu, anayejulikana kwa jina lake la kisanaa kama Burna Boy, amekuwa msanii wa kwanza wa muziki wa Nigeria kufikia rikodi hiyo ambapo Odogwu amejinyakulia zaidi ya bilioni N3 za mauzo ya tiketi pekee.


Tiketi ziliuzwa kwa bei ya chini kwa dola $80 na wastani wa dola $350 huku tiketi za juu Zikiuzwa kwa dola $2,125. Kulingana na hesabu za Business Day kwa kutumia wastani wa mauzo ya N145,365.50 ambapo ni dola ($350) ikizidishwa na jumla ya uwezo kuchukua watazamaji unaopatikana katika uwanja wa huo 20,789, na kiwango cha ubadilishaji cha sasa cha fedha za kigeni nchini Nigeria N415.33 jumla yake ni $7,276,150 ambayo ni zaidi ya N3,03022,090. .

Tamasha hilo la kihistoria lililotumia takribani saa 2 liliruka moja kwa moja kwenye Youtube na kupata watazamaji zaidi ya 81,000 mashabiki kutoka nchi tofauti zikiwemo Nigeria, Uingereza, Australia na Canada. Burna Boy alifungua onyesho akiwa amevalia koti jeusi la wabunifu na suruali nyeusi ili kuendana na kubadilisha mavazi ya kupendeza alipokuwa akiimba nyimbo kutoka kwa albamu zake za African Giant na Twice as Tall.


Burna Boy anaungana na Michael Jackson, Elvis Presley, The Beatles, Adele, Rihanna, Jay-Z, Justin Bieber, Mariah Carey kwenye orodha ya Wasanii, ambao wameuza tiketi zote katika uwanja maarufu zaidi duniani.


Mwaka huu pekee msanii wa huyo wa Afro-Fusion ameongoza matukio katika miji ya Amsterdam, Dublin, Manchester na Rotterdam.
Forexmart

Comments