Msanii wa muziki wa RnB Juma Jux kutokea kiwanda cha muziki wa Bongo fleva ameendelea kutanua wigo wa biashara zake Kimataifa ambapo siku ya jana ameingia kwenye headlines kwa mara nyingine baada ya kuchapisha video katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha akiwa kwenye mualiko wa chakula cha jioni na Boss na mwanafamilia waanzilishi wa Hennessy, bwana Maurice R. Hennessy.
Kwenye mualiko huo, Jux pia amepewa zawadi ya chupa ya Hennessy iliyoandikwa jina lake, inayokadiriwa kuwa na thamani ya Euro 3,100 ambazo ni zaidi ya Shillingi Milioni 7.5 kwa fedha za hapa nyumbani.
African Boy anameeleza kuwa safari zake nje ya nchi zitakwenda kufungua fursa nyingi za kibiashara kwake na vijana wengi hapa nchini.


Comments
Post a Comment