Skip to main content

Erik ten Hag Asisitiza kuwa Ronaldo Hauzwi Manchester United

Kocha Mkuu wa Manchester United, Erik Ten Hag amesema mchezaji wa klabu hiyo na taifa la Ureno nyota Cristiano Ronaldo hatouzwa kwa sababu klabu hiyo ina malengo naye kwa ajili ya msimu ujao. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi za kuwa Ronaldo anahitaji kuondoka United.


Ten Hag ameongeza kuwa “Niliongea na Ronaldo kabla ya haya mambo kujitokeza na maongezi yetu yalikuwa mazuri na niko na mpango naye wa kumtumia tunataka kupate mafanikio tukiwa naye, kama nilivyosema mwanzo Ronaldo hauzwi”

Forexmart

Aidha Erik ten Hag amethibitisha kuwa Harry Maguire atasalia kama nahodha wa Manchester United kwa msimu ujao na haoni kumbakiza nahodha kama suala muhimu.

Huku United wakimwinda Lisandro Martinez msimu huu wa joto, Maguire atakabiliwa na ushindani zaidi katika nafasi yake na kumekuwa na uvumi kwamba Ten Hag anaweza kuteua nahodha mpya , Lakini Ten Hag amemuunga mkono Maguire kubaki na kitambaa hicho msimu huu.

“Harry Maguire ndiye nahodha. Ni lazima niwafahamu wachezaji wote, lakini ni nahodha aliyeimarika na amepata mafanikio mengi Sioni hili kama suala la muhimu zaidi” alisema.

Maguire anaweza acheze dakika chache dhidi ya Liverpool katika mechi ya kwanza ya kirafiki ya kujiandaa na msimu ujao kwa United ,  Bangkok, na Ten Hag anatazamia kuona jinsi timu yake itakavyopambana na adui anayemfahamu.


Comments