Skip to main content

Zuchu Afikia Rikodi Hii Instagram , Awatibua Mastaa Wa Kike Bongo

Zuhura Othman anayetambulika kwa jina lake la kisanaa kama Zuchu anazidi kupanda nafasi kila kukicha baada ya kufikisha wafuasi milioni 5 katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo sasa anakaribia kuwafikia wafuasi wa msanii mwenzake Nandy ambaye ana wafuasi milioni 6.6 katika mtandao huo.


Juma lililopita Zuchu alichapisha chapisho katika ukurasa wake wa instagram na kuwataka mashabiki zake kutomfanisha na msanii yoyote wa kike kutokea ukanda wa Afrika Mashariki na kudai kuwa kwa hatua aliyofika anapaswa kupambanishwa na wasanii wa kiume kwani anao uwezo mkubwa wa kuandika nyimbo na kutunga.

Niwashukuru Wazazi wangu ni kwa ajili yenu na Uwezo wa m/mungu tu .kwa uandishi wangu yafaa kuwekwa kwenye ligi za wanaume wadada wenzangu ntawaonea tu. Respectfully my pen game hard I could write for a guy and not notice. Releasing two songs this month,” - Zuchu.


Zuchu ambaye anatamba na nyimbo zake mbili mpya alizoziachia hivi karibuni "
Jaro" na "Fire" ndiye msanii pekee kutoka ukanda wa nchi zinazopatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na wafuasi wengi katika mtandao wa maudhui ya video wa Youtube akiwa na jumla ya wafuatiliaji milioni 2.

Mwaka 2021, Zuchu aliweka rikodi katika mtandao huo baada ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kutokea ukanda huu kufikisha wafuasi million 1 ndani ya miezi 11 tu tangu chaneli yake kufunguliwa katika mtandao huo , Zuchu pia aliweka rikodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa kike kutokea ukanda huu kufikisha watazamaji milioni 1 kwa video moja ndani ya masaa 22 na wimbo wake alioupa jina Sukari.

Comments