Zuhura Othman anayetambulika kwa jina lake la kisanaa kama Zuchu anazidi kupanda nafasi kila kukicha baada ya kufikisha wafuasi milioni 5 katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo sasa anakaribia kuwafikia wafuasi wa msanii mwenzake Nandy ambaye ana wafuasi milioni 6.6 katika mtandao huo. Juma lililopita Zuchu alichapisha chapisho katika ukurasa wake wa instagram na kuwataka mashabiki zake kutomfanisha na msanii yoyote wa kike kutokea ukanda wa Afrika Mashariki na kudai kuwa kwa hatua aliyofika anapaswa kupambanishwa na wasanii wa kiume kwani anao uwezo mkubwa wa kuandika nyimbo na kutunga. “ Niwashukuru Wazazi wangu ni kwa ajili yenu na Uwezo wa m/mungu tu .kwa uandishi wangu yafaa kuwekwa kwenye ligi za wanaume wadada wenzangu ntawaonea tu. Respectfully my pen game hard I could write for a guy and not notice. Releasing two songs this month ,” - Zuchu. Zuchu ambaye anatamba na nyimbo zake mbili mpya alizoziachia hivi karibuni " Jaro " na " Fire " ndiye msanii ...
Kocha Mkuu wa Manchester United, Erik Ten Hag amesema mchezaji wa klabu hiyo na taifa la Ureno nyota Cristiano Ronaldo hatouzwa kwa sababu klabu hiyo ina malengo naye kwa ajili ya msimu ujao. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi za kuwa Ronaldo anahitaji kuondoka United. Ten Hag ameongeza kuwa “Niliongea na Ronaldo kabla ya haya mambo kujitokeza na maongezi yetu yalikuwa mazuri na niko na mpango naye wa kumtumia tunataka kupate mafanikio tukiwa naye, kama nilivyosema mwanzo Ronaldo hauzwi” Aidha Erik ten Hag amethibitisha kuwa Harry Maguire atasalia kama nahodha wa Manchester United kwa msimu ujao na haoni kumbakiza nahodha kama suala muhimu. Huku United wakimwinda Lisandro Martinez msimu huu wa joto, Maguire atakabiliwa na ushindani zaidi katika nafasi yake na kumekuwa na uvumi kwamba Ten Hag anaweza kuteua nahodha mpya , Lakini Ten Hag amemuunga mkono Maguire kubaki na kitambaa hicho msimu huu. “Harry Maguire ndiye nahodha. Ni lazima niwafahamu wachezaji wote, lakini ni nahod...