Skip to main content

Posts

Otile Brown Athibitisha Kutengana Na Mpenzi Wake Muethiopia

Mwanamuziki kutokea nchini Kenya Otile Brown amethibitihsa kuachana na mpenzi wake anayejulikana kwa Jina Nabbayet raia wa Ethiopia. Otile ameweka wazi hayo kupitia Insta story yake kwa Kuandika kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na Nabbi walijaribu kusuluhisha changamoto walizokuwa wakizipitia lakini haikuwezekana hivyo kila mtu akaamua aendelee na maisha yake. Otile ameandika “Mimi na Nabbi hatuko pamoja tena, mara ya mwisho kuwa nae tulikuwa tunajaribu kutatua changamoto zetu lakini tukalidhia kutengana.” Hata hivyo licha ya kutengana huko Otile amesema kuwa “Nabbi ni mtu mwema sana , nitaendelea kumuheshimu , kumjali na kuwa na amani kati yetu. Namtakia maisha mema”

Harmonize Atangaza Kuhamia Kwenye Filamu

Mkurugenzi wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza kuingia kwenye fani ya uigizaji wa filamu muda wowote kuanzia sasa. Kondeboy ameweka wazi hilo kupitia Insta Story yake ambapo amebainisha kuwa filamu hiyo kwa mara ya kwanza itaoneshwa kupitia mtandao wa Ceek , Kampuni ambayo inajihusisha na masuala ya burudani kama kurusha matukio ya mubashara mtandaoni, kuandaa matamasha, kutengeneza headphones n.k Harmonize ameandika “Nimechoka kusubiri filamu yangu ya kwanza. Itakuwa kali sana, tukutane Ceek hivi karibuni jisajili sasa” - Harmonize

Diamond Platnumz Atua Nigeria Kimya Kimya , Akutana Na Jay Willz

  Jay Willz akiwa Na Diamond Platnumz Mwaka 2022 umeanza kwa kasi sana kwa mwanamuziki  Diamond Platnumz kutokana na kazi zake za Muziki , Baada ya kumaliza kolabo na The Ben kutoka nchini Rwanda Diamond sasa Amevuka mipaka mpaka nchini Nigeria. Nyota huyo ambaye ni mkurugenzi wa lebo ya muziki WCB Wasafi kwa sasa Yupo nchini Nigeria akiwa anakamilisha video na msanii wa muziki kutokea nchini humo anayeitwa  Jay Willz  ambaye anatamba na wimbo wake unaoitwa Medicine aliouachia tangu Agost 25, 2021. Kupitia ukurasa wake wa katika mtandao wa Instagram Jay Willz amechapisha picha akiwa na Diamond katika moja ya Eneo ambalo wanatayarisha  video Hiyo na kuambatanisha maneno yaliyosomeka “ Diamond Platnumz feat Rolly Boy Big 2022 ” Diamond Platnumz ametua Nchini humo kimya kimya  kukamilisha kideo hicho na Huku akiwa na shughuli zingine za kimuziki katika taifa hilo.

John Cena Achukua Nafasi ya Finn Balor , Sasa Kupambana Na Roman Reigns Agosti 21

Mkongwe wa WWE John Cena usiku wa Jana alirejea tena Kwenye kampuni hiyo Baada ya kukaa Nje ya mchezo Huo kwa Muda wa mwaka mmoja na nusu , Kurudi kwake kumeifanya WWE kurejea kwa Kishindo huku John akikiri kwamba Amerejea katika Mchezo huo kuuchukua Utawala wa Mashindano hayo Makubwa nchini Marekani. Baada ya tukio hilo Sasa Bingwa wa WWE Universal Champion Roman Reigns atakabiliana na John Cena hii ni baada ya John kusaini mkataba wa Kupambana na Mpinzani huyo mnamo Agosti 21. Awali Roman Reigns aligoma Kupigana na John Cena kwenye kipindi cha Smack Down wiki iliyopita na  kukubali kupambana na Mpinzani mwingine Finn Balor kisha John Cena akatokea na Kuchukua nafasi ya Finn hivyo Mpambano rasmi utakuwa Agosti 21 mwaka 2021.

Kanye West Atunukiwa Heshima Katika Jiji la Atlanta ' Julai 22 Yatajwa Kuwa Siku Ya KANYE WEST

Masaa machache Kabla ya Kanye West kuingia Jukwaani Katika Uzinduzi wa albamu ya DONDA, Rapa huyo alijikuta Akipokea heshima kutoka kwa uongozi wa Jiji la Atlanta kwa kumtunuku siku ya tarehe 22, Julai kila Mwaka katika jiji hilo kuwa siku ya KANYE WEST. Katika Uzinduzi wa Awali wa albamu hiyo Usiku wa Jana ' Wakaazi wa Jiji la Atlanta walifanikiwa Kuujaza uwanja wa Mercedes Benz kwa Lengo la kuisikiliza Albamu ya DONDA huku Kwa mara ya Kwanza baada ya Kitambo rapa Jay Z atasikika tena Katika moja ya Nyimbo zinazopatikana Katika albamu hiyo ' Pia mwanamama Kim Kardashian akiwa Ameongozana na Watoto wake North , Saint , Chicago , and Psalm walikuwepo Katika kuisikiliza Albamu hiyo. Kanye West alizaliwa huko Atlanta na aliishi Katika jiji hilo hadi Alipokuwa na miaka Mitatu kufuatia wazazi wake Kuachana.  Baba yake anaitwa Ray West, alikuwa mwandishi wa picha na Jarida la Atlanta na Mama yake, marehemu anaitwa Donda West, alikuwa Profesa wa Kiingereza katika Chuo Kikuu cha Clark ...

Leo Messi Kusaini Mkataba Mpya Barcelona Mpaka Mwaka 2026

 Rasmi sasa Klabu ya Barcelona Ina uhakika Asilimia 100 kumbakisha mchezaji Tagemezi wa klabu hiyo Leo Messi kwa kuwa Mshambuliaji huyo Yupo mbioni kusaini mkataba Mpya na Wanacatalunya hao ' Mkataba utakao mbakisha Uhispania mpaka Mwaka 2026. Habari za kuaminika Kutoka ndani ya Klabu zinasema kuwa Tayari makubaliano ya Awali kuhusu mkataba mpya Yalishafanyika hivyo Vimebakia vitu vichache na Rasmi watatoa tamko siku Chache zijazo. Mwanzo Messi alitaka Kusaini miaka 3 Kuitumikia miamba hiyo Ila sasa atasaini Miaka 5 itakayomweka Fc Barcelona mpaka mwaka 2026 huku akikubali Kupunguza mshahara Wake.

Diamond Platnumz Akutana na Snoop Dog Marekani

Nyota wa Bongofleva Diamond Platnumz Bado yupo nchini Marekani akiwa Katika Maandalizi ya Mwisho ya Album yake Ambayo Itatoka siku za Hivi karibuni. Akiwa nchini Humo Diamond Platnumz ameshakutana na Wasanii wengi Wakubwa na Siku ya Jana Alifanikiwa kukutana na Mkali wa Muziki wa Kufoka Legendari Snoop Dogg. Katika video Hii  Snoop Dog amemueleza diamond platnumz ni Kwa kiasi Gani Jamii yake Ya karibu Ilivyomkataa Kipindi Anaanza Muziki ' Mpaka sasa kufikia kuwa Mfano wa Kuigwa  na Wasanii wengine Chipukizi na Waliopo kwenye Muziki. TAZAMA MAZUNGUMZO YA DIAMOND NA SNOOP DOG

Sergio Ramos Afunguka Mwanzo Mwisho Sababu za Kuondoka Real Madrid

Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa nahodha wake Sergio Ramos ataondoka klabuni hapo katika dirisha la usajili la majira ya joto (Summer) baada ya kuhudumu klabuni hapo kwa miaka 16. Awali Madrid walituma ofa ya mwaka mmoja huku nyota huyo akitaka angalau mkataba wa miaka miwili. Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameweka wazi kuwa, wakati makubaliano ya mkataba mpya na Ramos hayakufikiwa na kusisitiza kuwa Sergio Ramos ataendelea kukaribishwa tena klabuni hapo kwa siku za usoni. Katika sherehe za kumuaga Sergio Ramos zilizofanyika Madrid siku ya jana. Ramos amefunguka ukweli wote ikiwemo taarifa ya kuomba apewe mkataba mpya tangu 2018 baada ya fainali za michuano ya UEFA mwaka huo , Lakini Perez alikuwa akitoa ahadi hewa. Unaambiwa katika zama za Perez hakuna Legend aliyestaafu akiwa na jezi ya Real Madrid. MKUTANO WA SERGIO RAMOS NA WAANDISHI WA HABARI Real Madrid walitaka kunipa mkataba mpya nami nilikubaliana nao, ukiwa na kipengele cha kupunguza mshahara kwa 10% , Sikuwa na...

Diamond Platnumz Awakimbiza Wizkid , Burna Boy Tuzo za BET

Nyota wa muziki kutokea nchini Tanzania, Naseeb Abdul Juma maarufu kwa jina Diamond Platnumz ameonekana kupata muitikio mkubwa kwenye post za wasanii wa Afrika aliokutana nao kwenye kipengele cha "Best International Act" kwenye tuzo za BET 2021. Diamond amepata muitikio wa idadi kubwa ya maoni na 'likes' kwenye post za Instagram za wiki iliyopita za ukurasa wa 'Bet Africa' tofauti na wasanii wengine wa Afrika aliokutanishwa nao kwenye kipengele hicho cha tuzo. Diamond akiwa ni msanii pakee kutokea Afrika Mashariki kuteuliwa kuwania tuzo hizo, wasanii aliokutanishwa nao kutoka Afrika ni pamoja Burnaboy, Wizkid. Kwenye kupengele hicho cha 'Best International Act', Diamond Platnumz mbali na Diamond  kukutana na wasanii hao kutokea nchini Nigeria pia amekutanishwa na Aya Nakamura (France), Emicida (Brazil), Headie One (Uk), Young T & Bugsey (Uk) na Youssoupha (France). Hii ndiyo Orodha ya Wasanii Wanao Wania Tuzo hii Na Diamond Platnumz Hata...

Zuchu Auwasha Moto Katika Tamasha la Siku ya Mwafrika Duniani

Kila ifikapo tarehe 25 mwezi Mei kila mwaka ni kumbikizi ya siku ya mwafrika Duniani , Siku hii ni maalumu kwa Waafrika wote Duniani kukumbuka kuwa tarehe 25/5/1963 nchi 32 za Afrika zilisaini mkataba wa umoja wa Afrika (AU) wa kuzidi kushikamana na kuimarisha amani katika kujipatia uhuru kutoka kwa wakoloni kwa kipindi hicho. Katika kuidhimisha siku hii kubwa MTV Base Africa Wakajitoa kuwaburudisha waafrika wote Duniani katika tamasha walilolipa Jina Africa Day Concert ambapo lilifanyika mubashara kupitia chaneli ya youtube ya Mtv Base Africa huku kauli mbiu ikiwa ni mapambano kuutokomeza ugonjwa wa malaria. Katika tamasha hilo wasanii kutoka mataifa mbalimbali walipata nafasi ya kutumbuiza akiwemo mwanadada Zuchu kutokea tasnia ya muziki wa Bongofleva na kwenye video hii , ni kipande kifupi kikionyesha sehemu ya kazi aliyofanya msanii huyo. Wasanii wengine waliotumbuiza katika Tamasha hilo ni pamoja na ;- 1. @bahatikenya Bahati Akitumbuiza , Afric...