Mwanamuziki kutokea nchini Kenya Otile Brown amethibitihsa kuachana na mpenzi wake anayejulikana kwa Jina Nabbayet raia wa Ethiopia. Otile ameweka wazi hayo kupitia Insta story yake kwa Kuandika kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na Nabbi walijaribu kusuluhisha changamoto walizokuwa wakizipitia lakini haikuwezekana hivyo kila mtu akaamua aendelee na maisha yake. Otile ameandika “Mimi na Nabbi hatuko pamoja tena, mara ya mwisho kuwa nae tulikuwa tunajaribu kutatua changamoto zetu lakini tukalidhia kutengana.” Hata hivyo licha ya kutengana huko Otile amesema kuwa “Nabbi ni mtu mwema sana , nitaendelea kumuheshimu , kumjali na kuwa na amani kati yetu. Namtakia maisha mema”