Zuhura Othman anayetambulika kwa jina lake la kisanaa kama Zuchu anazidi kupanda nafasi kila kukicha baada ya kufikisha wafuasi milioni 5 katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo sasa anakaribia kuwafikia wafuasi wa msanii mwenzake Nandy ambaye ana wafuasi milioni 6.6 katika mtandao huo. Juma lililopita Zuchu alichapisha chapisho katika ukurasa wake wa instagram na kuwataka mashabiki zake kutomfanisha na msanii yoyote wa kike kutokea ukanda wa Afrika Mashariki na kudai kuwa kwa hatua aliyofika anapaswa kupambanishwa na wasanii wa kiume kwani anao uwezo mkubwa wa kuandika nyimbo na kutunga. “ Niwashukuru Wazazi wangu ni kwa ajili yenu na Uwezo wa m/mungu tu .kwa uandishi wangu yafaa kuwekwa kwenye ligi za wanaume wadada wenzangu ntawaonea tu. Respectfully my pen game hard I could write for a guy and not notice. Releasing two songs this month ,” - Zuchu. Zuchu ambaye anatamba na nyimbo zake mbili mpya alizoziachia hivi karibuni " Jaro " na " Fire " ndiye msanii ...